Baa la njaa Sudan Kusini lapungua japo maelfu bado hawana uhakika wa chakula-WFP/UNICEF/FAO

21 Juni 2017

Baa la njaa limepungua Sudan kusini baada ya juhudi kubwa za kibinadamu za kulikabili , umesema uchambuzi wa pamoja uliotolewa Jumatano na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, shirika la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la chakula na kilimo FAO.

Hata hivyo hali inasalia kuwa mbaya nchini humo huku idadi ya watu wasio na uhakika wa chakula kila siku ikiongezeka na kufikia milioni 6 hivi sasa kutoka watu milioni 4.9 mwezi Februari, hii ikielezwa kuwa ni kiwango kikubwa kabisa cha kutokuwa na uhakika wa chakula kuwahi ushuhudiwa nchini Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa mashirika hayo matatu baa la njaa halipo tena kwenye maeneo ya Leer na Mayandit , jimbo la Unity ambako baa hilo lilitangazwa mwezi Februari. Serge Tissot mwakilishi wa FAO Sudan Kusini anasema pamoja na mafanikio hayo bado watu 45,000 wanahaha kwa njaa

(SAUTI YA SERGE)

“Sababu kubwa ni kuzorota kwa usalama katika maeneo mengi , awali kulikuwa na majimbo matatu tu yaliyokuwa na vita sasa kuna matatizo ya usalama karibu kila mahali Sudan kusini , hivyo kuna wakulima wachache wanaolima na kuna chakula kidogo .”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter