Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusaidie wakimbizi kwani wanachoomba ni kidogo- Guterres

Tusaidie wakimbizi kwani wanachoomba ni kidogo- Guterres

Idadi ya wakimbizi duniani ikifikia milioni 65.6 mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka jamii ya kimataifa ionyeshe ukarimu kwa kuwasaidia.

Katika ujumbe wake wa siku ya wakimbizi duniani hii leo, Guterres amesema wakimbizi hao aliosema ni majasiri, wanachoomba si kikubwa bali ni kitu kidogo tu cha kuwawezesha kuishi salama na kujikimu maisha yao.

Amesema licha ya machungu ya kukimbia na kuacha kila kitu..

(Sauti ya Guterres)

“Bado hawajapoteza ndoto za watoto wao au kukata tamaa ya hamu yao ya kuwa na mustakhbali bora. Wanaoomba kitu kidogo, usaidizi wako katika wakati ambao wanahitaji zaidi na mshikamano wetu.”