Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimetumikishwa kama kahaba, nashindwa kujinasua-Joy

Nimetumikishwa kama kahaba, nashindwa kujinasua-Joy

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inasema mamilioni ya watoto wanavuka mipaka ya kimataifa wakikimbia vurugu na migogoro, majanga au umaskini wakitumainia kupata maisha bora ugenini.

Shirika hilo linasema katika mwaka 2015 - 2016, Idadi ya watoto wakimbizi na wahamiaji waliotenganishwa na wasioambatana na wazazi wao ilifikia 300,000 kutoka nchi 80 ikilinganishwa na 66,000 katika mwaka 2010 – 2011.

Watoto hao wasipopata fursa ya kusafirishwa kisheria, wanajikuta mikononi mwa walanguzi. Mmoja wa watoto hao ni  msichana nayefahamika kwa jina moja Joy,  kutoka Nigeria. Ungana na Selina Jerobon katika makala ifuatayo, ambayo itakufafanulia zaidi aliyokumbana nayo ukimbizini.