Utii na utekelezaji wa sheria za kimataifa sio chaguo-Zeid

19 Juni 2017

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema utii na kuhakikisha utekelezaji wa sheria za kimataifa sio chaguo, akiongeza kwamba ukiukwaji wa haki za binadamu haukua dalili ya mgogoro baina ya Israel na Palestina, bali kichocheo cha mzunguko wa machafuko ambayo sasa yanaendelea kwa zaidi ya nusu karne.

Akiwasilisha ripoti Jumatatu mjini Geneva Uswis kuhusu ukiukwaji wa sheria za kimataifa katika eneo linalokaliwa la Wapalestina , Zeid amesema ili kuvunja mzunguko huo wa machafuko ni lazima suala la kukaliwa kwa Palestina na hofu ya Israel vipatiwe ufumbuzi.

Amesema anatambua kwamba kuheshimu haki za binadamu ni njia ambayo itawatoa watu kwenye machafuko hayo, na kuweka mazingira ya amani , akiongeza kwamba hayo yatahitaji utashi wa kisiasa  na kujidhatiti kwa wadau wote.

Zeid amesema ripoti inaorodhesha visa vya pande zote kushindwa kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya tume za haki za binadamu , ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Kamisha mkuu wa haki za binadamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter