Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kingono vitani ni tishio la haki ya kuishi kiutu-Guterres

Ukatili wa kingono vitani ni tishio la haki ya kuishi kiutu-Guterres

Ubakaji na ukatili wa kingono vitani ni mbinu za kigaidi na za kivita zinazotumika kudhalilisha , kudharaulisha , kuharibu na mara nyingi kufanya kampeni ya kutokomeza watu wa kabila fulani.

Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono vitani, akisisitiza kwamba siku hii ni ya kuwaenzi wanawake, wasichana, wanaume na wavulana walioathirika na ukatili huo na kusisitiza jukumu la kimataifa katika kuukomesha.

Ameongeza kuwa ukatili wa kingono vitani ni tishio la haki ya kila mtu ya kuishi kiutu na kwa binadamu wote kuwa na amani na usalama. Amesema Umoja wa mataifa unafanya jujudi zote kushughulikia mizizi ya ukatili huo huku ukizichagiza nchi kuchukua hatua kumaliza ubaguzi wa kijinsia.