Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tujiandae kabla ya ukame ili kuokoa wakulima- FAO

Tujiandae kabla ya ukame ili kuokoa wakulima- FAO

Huko Roma, Italia kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kunafanyika semina ya kimataifa kuhusu ukame na kilimo ambapo serikali na wadau wa kilimo wametakiwa kuachana na mtindo wa kusubiri ukame ndio wachukue hatua za kusaidia wananchi.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema tabia hiyo ina madhara makubwa akitolea mfano ukame nchini Somalia mwaka 2011 uliosababisha watu zaidi ya 250,000 kufa kwa njaa.

Amesema ingawa ni vyema kusaidia waliokumbwa na njaa pindi ukame unapowakumba..

(Sauti ya Graziano)

“Kuwekeza katika maandalizi na kujenga uwezo wa kukabili ukame ni muhimu. Kwa kufanya hivyo nchi zinakuwa na uwezo wa kuchukua hatua haraka kabla hazijachelewa, ikimaanisha wakulima na jamii za vijijini wanaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kukabiliana na hali mbaya zaidi ya hewa pindi inapowakumba.”

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa shirika la hali ya hewa duniani, WMO Petteri Taalas amesema shirika lake hutoa mwongozo na taarifa za kisayansi ili kuimarisha huduma za kitaifa za kukabiliana na athari za ukame kwenye kilimo.