Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi wa Syria Muzoon aweka historia kuwa balozi mwema wa UNICEF

Mkimbizi wa Syria Muzoon aweka historia kuwa balozi mwema wa UNICEF

Katika kuelekea siku ya wakimbizi duniani hapo kesho , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limemteua Muzoon Almellehan, mwenye umri wa miaka 19 mwanaharakati wa masuala ya elimu na mkimbizi wa Syria kuwa balozi wake mwema mpya na mdogo kabisa.

Uteuzi huo unamfaya Muzoon kuwa mtu wa kwanza mwenye hadhi ya ukimbizi kuwa balozi mwema wa UNICEF. Muzoon, ambaye alikuwa akipokea msaada kutoka UNICEF alipokuwa akiishi kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jordan, anafuata nyayo za hayati Audrey Hepburn, aliyekuwa balozi mwema ambaye alisaidiwa na UNICEF pia alipokuwa mtoto.

Baada ya uteuzi huo Muzoon amesema “hata nilipokuwa mtoto nilijua elimu ilikuwa ufunguo wa mustakhbali wangu, hivyo nilipokimbia Syria kitu pekee nilichobeba ilikuwa ni bvitabu vyangu” na ameongeza

(SAUTI YA MUZOON)

“Kwangu elimu ni kila kitu, ni kitu ambacho kina tupa kila kitu, hatuwezi kuleta mabadiliko yoyote bila elimu. Elimu ni kama ufunguo ambao unafungua milango iliyo mbele yetu na kutupa fursa zaidi.”

Muzoon f alikimbia vita Syria pamoja na familia yake mwaka 2013, na akaishi kama mkimbizi kwa miaka mitatu Jordan kabla ya kupatiwa makazi nchini Uingereza.