Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapewa taarifa ya maendeleo Mali

Baraza la usalama lapewa taarifa ya maendeleo Mali

Mwezi huu inatimia miaka miwli tangu kutiwa saini mkataba wa amani ulitotumainiwa kuwa wa kihistoria nchini Mali.

Baraza la usalama Ijumaa ya leo limepewa taarifa ya hatua zilizopigwa nchini humo na changamoto ambazo bado zinaendelea.

Umoja wa Mataifa ulianzisha operesheni Mali ili kusaidia taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi na wanamgambo kwenye itikadi kali kudhibiti eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, Mahamat Saleh Annadif amesema katika miezi ya karibuni kumekuwa na hatua kubwa zilizopigwa katika utekelezaji wa mkataba huo wa amani wa Juni 2015 na makubaliano ya maridhiano yaliyotiwa saini na upande wa serikali na makundi ya waasi. Anafafanua baadhi ya hatua hizo zilizopigwa

(SAUTI MAHAMATT)

"Mkutano wa umoja wa kitaifa ulifanyika katika hali nzuri, na katiba kwa ajili ya amani, umoja na muungano kwa sasa inaandaliwa. Pili: mamlaka ya serikali ya mpito ilianzishwa katika maeneo matano yanayotia wasiwasi, angalau kasi yao ya kazi ni tofauti kati ya eneo moja hadi jingine . Wakati huu, hakuna tena msuguano wa kisiasa bali masuala ya kiufundi ".