Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Mtoto Zanzibar

Mahakama ya Mtoto Zanzibar

Mwaka 1989, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC. Mkataba huu ulilenga kusimamia misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambayo ni Kuishi, Kuendelezwa, Kushirikishwa na Kulindwa. Ibara ya 3 ya mkataba huo inagusia haki ya mtoto kwenye masuala yote ya kisheria, ikitaka haki ya mtoto kulindwa. Mathalani haki ya mtoto inapopindishwa, suala lake lifikishwe kwenye vyombo vya sheria ili haki ipatikane. Suala la faragha na uhuru wa kutoa maoni bila vitisho. Hilo limefanyika huko Tanzania-Zanzibar na ndio mada kuu hii leo ambayo Joseph Msami ndio mwenyeji wako.