Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nusu ya watoto hawana fursa ya kufurahia utoto wao na baba zao-UNICEF

Zaidi ya nusu ya watoto hawana fursa ya kufurahia utoto wao na baba zao-UNICEF

Zaidi ya nusu au asilimia 55 ya watoto wa umri wa miaka 3 na 4 katika nchi 74 duniani ambao ni takribani watoto milioni 40 wana kina baba ambao hawachezi nao au kushiriki katika shughuli za elimu yao ya awali , kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa Ijumaa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Laurence Chandy mkurugenzi wa UNICEF wa kitengo cha takwimu, utafiti na sera amesema hali hii inadhihirisha kwamba kina baba wengi wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na jukumu muhimu katika miaka ya awali ya watoto wao.

Ameongeza kuwa ni lazima kuondoa vikwazo vinavyowazuia kina baba hao kuwapa mazingira muafaka watoto wao ikiwemo upendo, muda wa kucheza nao, ulinzi na lishe bora.

UNICEF imetoa uchambuzi huu katika kuelekea siku ya baba duniani ambayo itaadhimishwa Jumapili Juni 18 katika nchi 80 ikiambatana na hashtag #EarlyMomentsMatters ikichagiza kina baba kuwa na wajibu mkubwa kwa watoto wao.