Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hata nchi tajiri zahaha kutimiza SDGs-UNICEF

Hata nchi tajiri zahaha kutimiza SDGs-UNICEF

Mtoto mmoja kati ya watoto watano katika nchi zilizoendelea wanaishi katika umasikini, ilihali mmoja kati ya wanane hawana uhakika wa chakula, umebaini utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Utafiti huo ulioko katika ripoti ya UNICEF iliyochapishwa leo, unasema kwamba, nchi zenye uchumi wa kiwango cha juu zaidi duniani , zinahaha kuhakikisha ustawi wa watoto ambao ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs au ajenda ya 2030.

Ripoti hiyo inathibitisha kwamba nchi hizo 41 zinakabiliana na ukosefu wa usawa. Jose Cuesta ni mkuu wa ofisi ya UNICEF ya masuala ya uchumi na utafiti.

( Sauti Jose)

‘Nafikiri ujumbe muhimu hapa ni kwamba , kipato au kukua kwa uchumi pekee hakutawakomboa watoto katika madhila kadhaa. Sera thabiti, na uwezo wa kukabiliana na majanga pia ni vigezo muhimu katika kuwezesha ustawi wa watoto.’’