Nyanya apanda mbegu ya imani kwa wakimbizi-Uganda

14 Juni 2017

Mgogoro na njaa nchini Sudan Kusini ukiendelea, wananchi wamelazimika kukimbilia nchi jirani zikiwemo Uganda, Sudan, Ethiopia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya kati kusaka hifadhi. Jamii nchini Uganda zimetoa mfano wa kuigwa kwa kufungua nyumba zao na kuwakirimu wakimbizi hao.

Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon anakutana na mwanamke mwenye umri wa miaka 70 katika wilaya ya Yumbe, karibu na makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda. Ungana naye kwa undani zaidi...