Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki na sauti za watu wenye ulemavu vijumuishwe kwenye SDGs- Hungbo

Haki na sauti za watu wenye ulemavu vijumuishwe kwenye SDGs- Hungbo

Mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu COSP10, umeanza leo mjini New York, Marekani ukiwaleta pamoja nchi wanachama 173 wa mkataba huo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu idara ya uchumi na masuala ya kijamii ya umoja huo DESA Wu Hungbo amewaambia washirikai zaidi ya 1000 kuwa mkutano huo unafanyika wakati muhimu.

( Sauti Hungbo)

‘‘Wakati ambapo jumuiya ya kimataifa inaongeza kasi ya juhudi ya ajenda ya 2030 jumuishi kwa kuzingatia mukatadha wa mkataba na majukumu mengine husika ya kimataifa.’’

Ameongeza kuwa COSP10 ina jukumu muhimu la kuhakikisha juhudi zote za maendeleo zinajumuisha haki na sauti za watu wenye ulemavu na kwamba.

(Sauti Hungbo)

‘‘Kukabiliana na aina kadhaa za ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu ni muhimu katika utekelezaji wa ajenda ya 2030 na kufanikisha SDGs kwa watu wote.’’