Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazakhstan ni muhimu katika ustawi wa Asia ya Kati- Guterres

Kazakhstan ni muhimu katika ustawi wa Asia ya Kati- Guterres

Umoja wa Mataifa umesema unapenda kuona eneo la Asia ya Kati linakuwa na amani na ustawi, hivyo ushirikiano zaidi unatakiwa baina ya nchi za ukanda huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuanza ziara yake nchini Kazakhstan.

Amesema udau kati ya Umoja wa Mataifa na Kazakhstan ni muhimu katika kufanikisha matarajio hayo katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Bwana Guterres ambaye anashiriki mkutano wa ushirikiano wa nchi za ukanda wa Ulaya na Asia uitwao Shanghai Cooperation Organisation au SCO pamoja na maonyesho ya biashara ya 2017 EXPO2017 ambayo amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Natumai yatakuwa ni muhimu sana katika ahadi yetu kwenye maendeleo endelevu hasa kuhusiana na jambo ambalo ni muhimu sana la mabadiliko ya tabianchi na bila shaka ni suala la nishati.”