Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi wa kimataifa ufanyike dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu DRC- Zeid

Uchunguzi wa kimataifa ufanyike dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu DRC- Zeid

Tuna wajibu kwa wahanga na jukumu la kutuma ujumbe kwa wahusika wa uhalifu wa ukiukaji wa haki za binadamu na, kwamba tunawafuatilia na jumuiya ya kimataifa inatia uzito kuhakikisha ukwepaji wa sheria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC unakomeshwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kauli hiyo imetolewa Ijumaa na kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein, akitoa wito kwa baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis kuanzisha uchunguzi wa kimataifa dhidi ya kuenea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili mwingine kwenye majimbo ya Kasai Kati na Kasai Oriental nchini DRC, ikiwemo kupatikana kwa makaburi ya pamoja takribani 42.

Ukiukaji mwingine ni pamoja na ukatili wa kingono, na mauji yakiwemo ya watoto. Tangu Agost 2016 watu milioni 1.3 wamekuwa wakimbizi wa ndani huku wengine 30,000 wamelazimika kulihama jimbo la Kasai na kukimbilia Angola. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RAVINA)