Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mama akisema ndio hakuna atakayesema hapana!

Mama akisema ndio hakuna atakayesema hapana!

Mila na desturi za baadhi ya makabila duniani zinataka mtoto wa kike aolewe tu punde baada ya kubalehe. Msingi mkuu wa mila hii ni fikra potofu ya kwamba mtoto wa kike hana msaada wowote kwa familia yake zaidi ya kwenda kuolewa na kuzaa watoto. Miongoni mwa makabila hayo ni wasamburu huko Afrika Mashariki na hususan nchini Kenya ambako mila hiyo imekuwa kikwazo kwa wanawake. Hata hivyo mwanamke mmoja ameweza kuvunja mila hiyo na kuwezesha watoto wake kusoma hadi hata kupata shahada ya uzamivu yaani Phd licha ya vikwazo kutoka kwa kakazake. Je nini kilitokea? Assumpta Massoi amezungumza na Dkt. Josephine Kulea, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wasichana wa jamii ya Samburu kutoka chini Kenya ambaye ndiye mnufaika wa hatua ya mama yake kukataa mila ya wasamburu na kuwapeleka shule.