Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wazi kuwa wanawake ndio wanaoteseka zaidi katika vita-Owusu

Ni wazi kuwa wanawake ndio wanaoteseka zaidi katika vita-Owusu

Jukwaa la wazi Kimataifa kwa ajili ya Wanawake linafanyika wiki hii jijini Juba, Sudan Kusini kujadili usawa wa kijinsia, ukatili wa kijinsia, ubaguzi, ndoa za shuruti na za mapema ili hatimaye kuwawezesha wanawake katika ngazi zote kuleta amani.

Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Eugene Owusu amesema mwaka 2000 baraza la usalama kwa mara ya kwanza lilipitisha azimio nambari 1325, baada ya kutambua umuhimu wa mchango wa wanawake katika kuzuia vita, kulinda na kuleta amani na masuala yote yanayohusu amani, azimio ambalo limepewa mamlaka ya kupigia chepuo.

Amesema katika siku ya mwisho ya mkutano huo ambao utajumuisha wadau wa kimataifa, watetezi wa wanawake, wakuu wa madhehebu ya kidini, wanawake wa Sudan Kusini na wadau wengine ...

(Sauti ya Owusu)

"Seti ya mapendekezo yataletwa mbele ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hapa Sudan Kusini kwa ajili ya utekelezaji wa haraka, na mapendekezo haya yatafuatiliwa na kukaguliwa kwa karibu mara kwa mara, ili kuhakikisha utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na wadau wote ikijumuisha wakuu wa Umoja wa Mataifa."