Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahari ni ajira kwa vijana-Freeman

Bahari ni ajira kwa vijana-Freeman

Vijana waweza kukuza kipato kupitia bahari na kufanikisha kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs amesema mwakilishi ni mwakilishi wa kudumu wa vijana wa Kenya katika ofisi za Umoja wa Mataifa Samuel Freeman.

Katika mahojiano na idhaa kandoni mwa mkutano wa siku tano kuhusu bahari unaondelea mjini New York Marekani Bwana Freeman amesema uwepo wao katika mkutano ni manufaa kwa vijana nchini Kenya na Afrika kwa ujumla na akitaja namna wanavyoweza kunufaika na habari amesema .

( Sauti Freman)

Amesema uchafuzi baharini ni miongoni mwa mada ambazo wanazitilia mkazo ili kupata suluhisho katika masuala kama vile kukabiliana na magonjwa yatokanayo na uchafuzi huo.