Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika inahitaji mageuzi katika amani-Mongella

Afrika inahitaji mageuzi katika amani-Mongella

Baada ya kuundwa na kukutana mjini New York Marekani kwa siku tatu, mtandao wa viongozi wanawake wa Afrika, umeazimia pamoja na mambo mengine kuhakikisha bara hilo linajikomboa katika migogoro kisha kupiga hatua za kimaendeleo.

Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni mwanasiasa nguli kutoka Tanzania, aliye pia mwanaharakati wa wanawake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi Gertrude Mongella,aliyemweleza Joseph Msami muda mfupi baada ya mkutano kuwa ipo fursa ya ukombozi wa wanawake katika maeneo yenye migogoro.

Amesema utatuzi wa amani na maendeleo ya Afriak unategemea zaidi wanawake, awali anaeleza upekee wa mtanadao huo wa wanawake viongozi wa Afrika