Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazibagui- Mugabe

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazibagui- Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amehutubia mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya bahari jijini New York, Marekani akisema kuwa ubia hasa usaidizi wa kiufundi ni muhimu ili kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yatokanayo na uchafuzi wa bahari.

Amesema hata hivyo kwa nchi yake ubia huo hasa katika kutelekeza lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu unakumbwa na kikwazo kutokana na vikwazo vilivyowekewa nchi yake ambavyo amesema si halali.

Rais Mugabe amesema..

(sauti ya Mugabe)

“Madhara ya mabadiliko ya tabianchi, hayabagui. Hebu na wasikilize hilo! Madhara ya mabadiliko ya tabianchi hayabagui. Hivyo ondoeni vikwazo vyenu.”

Rais Mugabe amewaeleza washiriki kuwa ingawa nchi yake haijazingirwa na bahari bado uharibifu na uchafuzi kwenye bahari una madhara kwa nchi zote kwa kuzingatia jinsi bahari zinavyotegemewa katika masuala ya tabianchi, usafirishaji na mlo.

Lengo namba 14 linataka uhifadhi endelevu wa bahari na matumizi endelevu ya viumbe vya bahari.