Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya mazingira duniani, asili ilindwe ili kulinda dunia:UNEP

Siku ya mazingira duniani, asili ilindwe ili kulinda dunia:UNEP

Utangamano na asili ndiyo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa leo kote duniani ikipigia chepuo uhifadhi na ulinzi wa maliasili za mazingira kwa mustakabali bora wa viumbe na sayari.

Akizungumiza siku hiyo K atibi Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bahari ,ardhi, misitu , maji na hewa tunayovuta ni mazingira yetu ambayo ni viungo muhimu katika sayari dunia.

( Sauti Guterres)

‘‘Katika Siku ya Mazingira Duniani na kila siku hebu tuungane na asili

hebu tuthamini dunia inayotulinda.’’

Kwa upande wake Mkuu wa mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa UNEP Erick Solheim amesema licha ya changamoto kadhaa kuna fursa za kuboresha maisha katika sayari akisema.

( Sauti Erick)

‘‘Tunaishi katika kipindi ambacho kuna fursa nyingi za kuwa na mazingira bora , tunapaswa kuzitumia. Hebu tuifanye sayari kuwa na furaha tena.’’

Nchini Tanzania, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema lazima kuzingatia kanuni za kuhifadhi mazingira kwa kuwa..

(Sauti ya Mama Samia)