Bahari ina uhusiano na kila mmoja wetu inatufanya tuishi-Guterres

5 Juni 2017

Bahari ina uhusiano na kila mmoja wetu, inatufanya tuendelee kuishi, lakini uhusiano huo sasa uko mahskani kuliko wakati mwingine wowote.

Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatatu katika mkutano maalumu ulioanza leo Juni 5 kuhusu masuala ya bahari na hasa lengo la maendeleo endelevu nambari 14.

Guterres amesema mkutano huo utakaomalizika Juni 9 ni wa kuchukua hatua ya pamoja dhidi ya ulinzi wa mali asili hasa bahari na sayari yetu kwa sababu..

(SAUTI YA GUTERRES )

“Bahari inatoa chakula, nishati, maji, ajira na faida za kiuchuni katika kila nchi hata zile zisizo na bahari. Ni muhimu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na ni rasilimali muhimu kwa ajili ya maendeleo endelevu."

Ameongeza uhusiano huo uko katika tiso kubwa sasa kwa sababu nyinmgi ikiwemo uchafuzi wa mazingira, uvuvi wa kupindukia na mabadiliko ya tabia nchi hivyo amependekeza hatua za kuchukuliwa na kila serikali

(SAUTI YA GUTERRES )

"Hatua ya kwanza ni kumaliza utenganishaji bandia baina ya mahitaji ya kiuchumia na afya ya bahari, pili tunahitaji kuchagiza uongozi imara wa kisiasa na ubia mpya, tatua lazima tutafsiri kwa ufadhili utashi wa kisiasa kwa ajili ya ajenda ya 2030, mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi na ajenda ya Adiss ababa ya kuchua hatua.”

Amesema hatua ya nne ni kupanua wigo wa ufahamu, kuwa na takwimu bora, taarifa na uchambuzi na mwisho ni ni lazima kubadilishana uzoefu mzuri katika kulinda bahari.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter