Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin, amefariki dunia hii leo. Alikuwa na umri wa miaka 68.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kushtushwa na kifo hicho akisema kuwa Babatunde alikuwa bingwa wa utetezi wa ustawi wa wanawake na wasichana.

Taarifa zaidi tutakuletea baadaye.

image
Kutoka ukurasa wa Twitter wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa punde tu baada ya kutangazwa kwa taarifa za kifo cha Dkt. Babatunde.