Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali shambulio la ugaidi liliotokea jana mjini London chini Uingereza na kusababisha vifo na mejeruhi kadhaa.
Vyombo vya habari vimeripoti kwamba watu saba wamefariki dunia, zaidi ya 40 wakijeruhiwa baada ya washambuliaji kuingia ndai ya umati wa watembea kwa miguu katika daraja kuu mjini London.
Katika taarifa yake kupitia msemaji wa Katibu Mkuu, Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa za wahanga wa shambulio hilo na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi .
Amesema ana matumaini kwamba wahusika wa uhalifu huo usio na uhalali watafikishwa kwenye mkono wa sheria hima na kueleza mshikamano wake na watu na serikali ya Uingereza katika kukabiliana na ugaidi na misiamamo mikali.
Katibu Mkuu amesema ugaidi ni tatizo kote duniani linalohitaji mshikamano wa jumuiya ya kimataifa katika kuwafikisha katika mkono wa sheria wanaotumia mbinu zilizo kinyume na binadamu na kusisitiza kuwa ni muhimu kulinda na kupigia chapeo haki na utu ambao magaidi wanataka kuutokomeza.