5 Juni 2017
Utatuzi wa amani katika maeneo yenye migogoro na ukombozi wa wanawake katika maeneo hayo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa na mtandao wa viongozi wa Afrika waliohitimisha mkutano wao mwishoni mwa juma mjini New York Marekani.
Katika mahojiano na idhaa hii Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi Getrude Mongella ambaye ni mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa wanawake kutoka Tanzania amesema baada ya mkutano huo , mtandao huo utahakikisha wanawekeza kuhakikisha sauti za wanawake katika nchi zenye migogoro zinapazwa.
( Sauti Mongela)
Amesema wajibu wa mtandao wa wanawake viongozi wa Afrika katika kuhakikisha maendeleo barani humo ni.
(Sauti Mongela)