Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za matumizi ya tumbaku kwa jamii na watu binafsi

Athari za matumizi ya tumbaku kwa jamii na watu binafsi

Mei 31 kila mwaka ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  “Tumbaku- tishio dhidi ya maendeleo”.

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kwamba zaidi ya watu milioni 7 hufariki dunia kila mwaka huku ikigharimu familia na serikali takriban dola trilioni 1.4 kwa ajili ya matibabu na nguvu kazi.

Kwa mantiki hiyo WHO imeonyesha ni jinsi gani matumizi ya tumbaku yanatishia maendeleo katika taifa kote ulimwenguni na inatoa wito kwa serikali kudhibiti matumizi ya uraibu huo ikiwemo: kuzuia matangazo ya tumbaku, kuongeza kodi ya bidhaa hizo na kukomesha uvutaji wa bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma na ya kazi.