Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterees asikitishwa na upungufu wa chakula kwa wakimbizi

Guterees asikitishwa na upungufu wa chakula kwa wakimbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres,amesikitishwa na hatma ya maelfu ya wakimbizi wa Sahrawi nchini Algeria ambao watapunguziwa mgao wao wa chakula kutokana na ukosefu wa chakula.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bwana Guterres amesema usaidizi wa kibinadamu ikiwamo chakula ni muhimu kwa ukanda huo wa jangwa la Sahara ambapo utafiti wa hivi karibuni umeonyesha hali mabya ya lishe katika kambi ya wakimbizi hao huku wakimbizi  wakishindwa kufikiwa na masoko.

Katibu Mkuu ametaka wafadhili kutoa usaidizi kwa dharura kwa ajili ya kuwasadia makundi hayo.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP inahitaji kisai cha dola milioni 7.9 kwa ajili kuendelea kutoa usaidizi kwa kipindi cha miezi sita ijayo

Upungufu wa fedha umesababisah  shirika la mpango wa chakula dunaini WFP kupunguza mgao kwawakimbiza hao kwa karibu mara 150 mwaka huu.