Maisha ya viumbe baharini ni moja ya wajibu wetu:FAO

2 Juni 2017

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari utafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New York Marekani .

Mkutano huo utakaoanza Juni 5 hadi 9 utaenda sanjari na maadhimisho ya siku ya bahari duniani ambayo kila mwaka hua Juni 8.

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO kauli mbiu ya mkutano huo ni “ubia kwa ajili ya utekelezaji wa leo nambari 14 la maendeleo endelevu ambalo ni maisha chini ya maji.

Katika mada hiyo mambo muhimu yatakayogusiwa ni jinsi gani ya kuhifadhi na kuwa na matumizi endelevu ya bahari na rasilimali za baharini kwa ajili maendeleo endelevu.

FAO linasema lina jukumu kubwa katika lengo nambari 14 ukizingatia kwamba aasilimia kubwa ya vioumbe vya baharini vitatumika kwa chakula na lishe na kuchangia katika maendeleo na mustakhbali wa watu wengi duniani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter