Wimbo watumika kuelimisha kuhusu Fistula

2 Juni 2017

Fistula ni ugonjwa ambao sasa ni mwiba kwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni mbili kuanzia Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Karibea hadi Amerika! Uchungu wa kupitiliza, kuchelewa kujifungua kwa wakati muafaka au kukatwa mrija wa kusafirisha mkojo wakati wa upasuaji wowote ule, vimetajwa kuwa ni sababu ya Fistula. Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA limesema kila mwaka wagonjwa wapya kati ya 50,000 hadi 100,000 huripotiwa ingawa kwamba ugonjwa huo waweza kuzuilika na zaidi ya yote kutibika kwa wale ambao wanao. Sasa UNFPA kupitia wanamuziki kutoka Senegal inatumia wimbo uitwao "Fistula Song" yaani wimbo wa Fistula ili kuelimisha umma kile cha kufanya. Assumpta Massoi amefuatilia kibao hicho kupitia makala hii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter