Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi hayapingiki-Guterres

Mabadiliko ya tabianchi hayapingiki-Guterres

Mabadiliko ya tabianchi hayapingiki na ni moja ya tishio kubwa katika ulimwengu wa sasa na mustakhbali wa sayari hii.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António  Guterres Ijumaa mjini St Petersberg Urusi akizitaka serikali kuendelea kushikamana na kutimiza wajibu wao katika utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi, akisistiza kwamba hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi hazizuiliki.

Na kuhusu jumuiya ya Marekani ambayo serikali yake imeamua kujiengua katika mkataba huo wa Paris, Guterres amesema anashawishika kwamba majimbo, miji , jumuiya za biashara, na asasi za kiraia za nchi hiyo zinaendelea kujihusiha na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha uchumi unaojali mazingira kwani huo ndio uchumi bora kwa mustakhbali wa dunia.