Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 50 wanaswa katika mtego wa kifo katika jangwa la Sahara

Wahamiaji 50 wanaswa katika mtego wa kifo katika jangwa la Sahara

Wahamiaji 44 kati ya 50 wanawake na watoto wamefariki dunia baada ya gari lao kuharibika katika jangwa la Sahara wakati wakielekea Libya kutoka Niger, taarifa za Umoja wa Mataifa zimesema leo. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Tukio hilo ambalo limetokea kati ya miji ya Agadez na Dirkou limetokana na joto kali na ukosefu wa maji ya kunywa na ni watu sita tu waliowahi kuokolewa katika kijiji cha mbali, ukingoni mwa jangwa la Sahara.

Taarifa imesema ni dhahiri kuwa vifo hivi vya kutisha ni matokeo ya tamaa ya walanguzi na wasafirishaji haramu ambao sasa wamepanua wigo wa mtego wa vifo kutoka bahari ya mideterenia kwenda jangwa la Sahara.

Leornard Doyle ni Msemaji wa Shirika la Wahamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM..

(Sauti ya Doyle)

"Walikuwa ni waGhana na waNigeria ambao wanajaribu kuvuka Libya kwenda Ulaya, na waathirika 6 walionusurika kati ya kundi lililofariki dunia kwa kiui, wamerejea na wanasaidiwa na IOM."