Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za upasuaji kwa wagonjwa Fistula -sehemu ya Pili

Hatua za upasuaji kwa wagonjwa Fistula -sehemu ya Pili

Katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mtaalamu wa afya kutoka mkoani Kagera nchini Tanzania  Dk Martin Lwabilimbo, tunaelezwa kile ambacho kinafanyika baada ya upasuaji wa kurekebisha Fistula, ugonjwa ambao unaondoa utu wa mwanamke. Mathalani Dokta Lwabilimbo amemweleza Nicolaus Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM mkoani humo kuwa, mgonjwa akishafanyika upasuaji anapatiwa pia ushauri nasaha ili aweze kurejea katika hali ya kawaida na kujitambua kwa kuwa awali kabla ya upasuaji huwa wanapoteza hata hali ya kujiamini na kutangamana na watu. Dkt. Lwabilimbo anaanza kwa kuelezea kinachofanyika baada ya upasuaji.