Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD yaelimisha uvuvi salama huko Indonesia

IFAD yaelimisha uvuvi salama huko Indonesia

Kuelekea mkutano wa kimataifa kuhusu bahari, tunaelekea huko nchini Indonesia, ambako mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD unashirikiana na jamii za wavuvi ili kulinda bahari ikiwemo matumbawe ambayo ni mazalia ya samaki.

Indonesia ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa uvuvi na uuzaji nje wa samaki na uvuvi wote huo hufanyika na wavuvi wadogo wadogo.

Kwa muongo mmoja uliopita, mahitaji ya samaki barani Asia yameongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo wavuvi haramu kutumia fursa hiyo kuvua samaki kinyume cha sheria na hatimaye kiwango cha samaki kilipungua.

IFAD inasema wavuvi hao wanatumia sumu au mabomu na hivyo hivi sasa wanawaelimisha wavuvi kufanya doria ili kulinda pwani mathalani hii ya Lembeh, mashariki mwa Indonesia.

Meneja mradi Angelique Rumondor amesema hivi sasa jamii imeimarisha doria na hivyo wana matarajio ya ongezeko la kiwango cha samaki.