Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na hatua katika vita dhidi ya AIDS, bado kuna pengo:Ripoti

Pamoja na hatua katika vita dhidi ya AIDS, bado kuna pengo:Ripoti

Wajibu wa kimataifa, kugawana jukumu la fedha, na mtazamo unaozingatia usawa miongoni mwa watu vimekuwa chachu kubwa ya mafanikio katika vita dhidi ya ukimwi, imesema ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iloyowasilishwa leo Alhamisi kwenye baraza kuu. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Ripoti hiyo “vita dhidi ya ukimwi kama chachu ya maendeleo endelevu na mabadiliko” inasema mkakati wa 90-90-90 umesaidia kupanua wigo wa upatikanaji wa tiba na dawa za kupunguza makali ya ukimwi jambo ambalo limepunguza maambukizi na vifo vya ukimwi kwa kiasi kikubwa .

Imeongeza kuwa mkakati wa kimataifa wa kupunguza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto umesaidia kukata azaidi ya nusu maambukizi ya HIV miongni mwa watoto.

Hata hivyo ikiwa imesalia chini ya miaka mine kufikia lengo la mwaka 2020 kuna shaka la kulifikia lengo imesema ripoti, kwani kumethibitika pengo kubwa katika kuzuia maambukizi ya HIV, upimaji na huduma za tiba katika kundi la watu wanaohitaji zaidi huduma hizo huku wanawake na wasichana wakiendelea kubeba mzigo mkubwa wa gonjwa hilo.