Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtandao wa wanawake viongozi Afrika wazinduliwa New York

Mtandao wa wanawake viongozi Afrika wazinduliwa New York

Mtandao wa wanawake viongozi barani Afrika umezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ukileta pamoja viongozi wa kisiasa na kitaaluma kwa lengo la kuchagiza ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa na ile ya 2063 ya Muungano wa Afrika, AU.

Lengo la mtandao huo unaochagizwa na Umoja wa Mataifa, AU na serikali ya Ujerumani ni kuangalia jinsi wanawake hao wanaweza kusongesha masuala ya amani, utawala bora na maendeleo kwa mujibu wa ajenda hizo.

Dkt. Asha-Rose Migiro,Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza ni miongoni mwa washiriki.

(Sauti ya Dkt. Asha-Rose)

image
Anna Mngwira ambaye aliwania urais nchini Tanzania mwaka 2015.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/A.Massoi)
Mshiriki mwingine ni Anna Mngwira ambaye aliwania urais nchini Tanzania mwaka 2015 kupitia chama cha ACT-Wazalendo ambaye amesema kupitia mtandao huu.

(Sauti ya Anna)