Mabadiliko ya tabianchi ni suala nyeti na kipaumbelele cha UM- Lajèák

31 Mei 2017

Lazima Umoja wa Mataifa uendeleze jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabiachi ili kuwafikia watu wa mashinani amesema Rais mteule wa kikao cha 72 cha baraza kuu la umoja huo Miroslav Lajèák, Lajèák [Mirosalv Laicheki] atakayeanza majukumu yake wakati wa kikao cha baraza hilo mwezi Septemba.

Akizungumza wakati wa mahojiano yake ya kwanza na waandishi wa habari  mjini New York Marekani,  muda mfupi baada ya kupitshwa na baraza kuu kushika wadhifa huo, Bwana Lajèák amesema muda umefika kwa jumuiya ya kimataifa kulipa kipaumbele suala la mabadiliko ya tabianchi akisema.

(Sauti Lajèák)

‘‘Naamini suala la mabadiliko ya tabianchi ni moja ya mambo ambayo Umoja wa Mataifa umefanya kazi nzuri sana, ni ajenda na kipaumbele cha umoja huo. Makubaliano ya Paris yamekuwa ya mafanikio , kwahiyo tunachohitaji kufanya ni kutekeleza na kuendelea na mchakato. Tabianchi ni miongoni mwa malengo 17 ya maendeleo endelevu, kwahiyo tunahitaji kuendeleza elimu kwani kwa baadhi ya nchi yaweza kuwa suala la kitaaluma tu , lakini kwa baadhi ya nchi ni la uhai.’’

 Kadhalika kiongozi huyo amesema ni muhimu Umoja wa Mataifa ukasaidia katika kuwafikia raia duniani hususani  kwa kuwa karibu nao kwani mataifa duniani bado yana imani na chombo hicho.

Bwana Lajèák ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Slovakia amesema suala la uhamiaji na changamoto zake litakuwa miongoni mwa vipaumbele vyake .

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter