Wapalestina wanastahili ajira zenye hadhi-ILO

31 Mei 2017

Miongo mitano ya kukaliwa imesababisha adha kubwa katika soko la ajira kwenye eneo linalokaliwa la Palestina na kufanya haja ya kufufua mchakato wa amani kuwa ni kitu cha lazima imesema ripoti inayotolewa kila mwaka ya shirika la kazi duniani ILO.

Ripoti hiyo ya 2017 “Hali ya wafanyakazi katika eneo linalokaliwa la Palestina” iliyotolewa leo Jumatano inadhihirisha vikwazo vya watu kutembea na shughuli za kiuchumi, vizuizi vya muda mrefu kwenye ukanda wa Gaza, kusuasua kwa mchakato wa amani na kuongezeka kwa ujenzi wa makazi ya Walowezi kuwa ni chachu ya kuendelea kuzorota kwa hali katika eneo hilo linalokaliwa.

Ripoti hiyo pia inatathimini ajira, hali ya soko la ajira na haki za wafanyakazi kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwemo Jerusalem Mashariki, Gaza na eneo linalokaliwa la Milima ya Golan.

Ripoti inatoa wito wa kuchapuza mchakato wa amani kwa lengo  la kuwa na suluhu ya mataifa mawili huku ikisisitiza kuwa Wapalestina wanastahili kuwa na ajira zenye hadhi kama walivyo watu wengine.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter