Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukaliwa kwa eneo la Palestina ndio chanzo cha zahma ya kibinadamu-UM

Kukaliwa kwa eneo la Palestina ndio chanzo cha zahma ya kibinadamu-UM

Wakati mwaka wa 50 ukikaribia tangu kuanza kukaliwa na Israel kwa eneo la wapalestina, ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA inasema sera na vitendo vya kukaliwa eneo la Palestina vinasalia kuwa chanzo kikubwa cha zahma na mahitaji ya kibinadamu katika eneo hilo.

Ripoti hiyo ya OCHA ya mwaka 2016 iliyotolewa Jumatano, inaeleza ni kwa nini kuna mipango ya kibinadamu katika eneo hilo, akitaja kwamba ukosefu wa ulinzi kwa raia wa Palestina dhidi ya machafuko, kutawanywa, vikwazo vya kupata huduma muhimu za maisha na ukiukwaji wa haki zingine vinaleta athari kubwa kwa watu wa Palestina hususani wanawake na watoto.

Ripoti imeongeza kuwa imeongeza kuwa mgawanyiko ndani ya himaya ya Palestina pia unachangia madhila. Hata hivyo imesema pamoja na kwamba mwenendo unatofautina kila mwaka lakini ukosefu wa ulinzi na uwajibikaji kwa ukiukwaji wa haki na sheria za kimataifa vinaendelea.