Guterres alaani shambulio la Baghdad

Guterres alaani shambulio la Baghdad

[caption id="attachment_318832" align="aligncenter" width="615"]hapanapaleiraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi la hivi karibuni katika mji wa Baghdad, nchini Iraq, ambalo limejeruhi raia wengi wakati wakiadhimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kwa kupitia msemaji wake, bwana Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia majeruhi afueni ya haraka.

Katibu Mkuu mesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushikamana na serikali na watu wa Iraq katika juhudi zao za kupambana na ugaidi na kutarajia kuwa wahusika wa vitendo hivyo watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.