Mwongozo wa kilimo salama Tanzania ni nuru kwa wakulima, wafugaji na wavuvi

30 Mei 2017

Nchini Tanzania kuanzia tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2017, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaanza kuelimisha watendaji wake katika halmashauri jinsi ya utekelezaji wa mwongozo mpya wa kilimo salama uliozinduliwa mwishoni mwa wiki. Mwongozo huo ukiambatana na wasifu wa kilimo salama kinachohimili mabadiliko ya tabianchi unalenga kupunguza, kuhimili na kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi. Katika kufahamu kile kilichomo kwenye mwongozo huo Assumpta Massoi amezugumza na Shakwaanande Natai,, Mkuu wa kitengo cha mazingira katika wizara hiyo na hapa anaanza kuelezea moja ya mbinu za kilimo kwenye mwongozo huo uliondaliwa kwa ushirikiano na wadau mbali mbali likiwemo shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa, FAO.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter