Tumbaku inaharibu mazingira- WHO

30 Mei 2017

Kuelekea siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani hapo kesho tarehe 31 mwezi Mei, shirika la afya ulimwenguni WHO limeweka bayana madhara mapya ya matumizi ya bidhaa hizo katika mazingira.

Wakizingatia maudhui ya mwaka huu kuwa Uvutaji sigara ni tishio kwetu sote, wataalamu wa WHO wamesema pamoja na kudhuru afya, kilimo cha tumbaku, uzalishaji wa bidhaa za tumbaku na utupaji wa bidhaa hizo baada ya matumizi kunaharibu mazingira.

Dkt. Vinayak Prasad ni afisa kutoka WHO akiongoza kampeni ya kutokomeza tumbaku anazungumzia kilichomo kwenye ripoti hiyo ya kwanza kabisa ya WHO kuhusu athari za tumbaku kwenye mazingira akisema kuwa ..

(Sauti ya Dkt. Prasad)

“Zao la tumbaku linafahamika kwa kusababisha mmomonyoko wa ardhi. Lakini tatizo ni kubwa zaidi tunapoangalia uzalishaji wa bidhaa zake. Kuna taka nyingi wakati wa uzalishaji, na bidhaa zinazotumiwa zinabakiza taka nyingi na tunaweza kuona karibu asilimia 40 ya taka zitokanazo na vishungi vya sigara maeneo ya pwani na mijini.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter