Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumu wa afya wa kujitolea wapelekwa Bas-Ulele kukabili Ebola:UNICEF

Wahudumu wa afya wa kujitolea wapelekwa Bas-Ulele kukabili Ebola:UNICEF

Katika juhudi za kudhibiti mlipuko wa karibuni wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wahudumu wa afya 145 wa kujitolea kutoka shirika la chama cha msalaba mwekundu la DRC na wahudumu wa afya ya jamii wamepelekwa katika jimbo la Bas-Ulele.

Wahudumu hao waliopatiwa mafunzo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, watatoa taarifa za kuokoa maisha kwa watu wa jimbo hilo ambao wengi wanaishi vijijini kuliko vigumu kufikika hasa mpakani na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Dr Tajudeen Oyewale,kaimu mwakilishi wa UNICEF nchini DRC amasema hakuna tiba ya Ebola hivyo kuzuia inasalia kuwa chaguo muhimu la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo, akisisitiza ushirikiano baina ya wahudumu wa afya na jamii husika ili jamii ipate taarifa muhimu kuhusu ugonjwa huo. Christopher Boulierac ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA BOULIERAC)