Mlo shuleni Kenya una mafanikio lakini uko mashakani:WFP

26 Mei 2017

Katika ziara yake ya kwanza nchini Kenya , mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ,David Beasley amepongeza mpango wa kitaifa wa mlo shuleni nchini humo unaotolewa na WFP na kufadhiliwa na mradi wa kimataifa wa Marekani, akisema umeleta mafanikio makubwa katika elimu.

Hata hivyo ameonya kwamba mradi huo sasa uko mashakani kutokana na mapendekezo ya upunguzaji wa bajeti yaliyotolewa na serikali ya Marekani. Beasely ambaye alitembelea shule ya msingingi kwenye eneo la Mathare mjini Nairobi inayofaidika na mradi huo , amewashukuru wahisani hasa serikali ya Marekani kwa kufanikisha mradi huo.

Kwa ushirikiano na serikali ya Kenya WFP imekuwa ikitoa mlo shuleni nchini huo kwa miaka 30 sasa. Jumla ya watoto milioni 2.2 katika nchi 11 ikiwemo Kenya wanafaidika na mradi wa WFP wa mlo shuleni.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter