Biashara isiyo rasmi inaweza kuinyanyua Afrika-FAO

25 Mei 2017

Shirika la chakula na kilimo FAO limewasilisha ripoti mpya kwenye mkutano mjini Kigali Rwanda Alhamisi, ikitoa muongozo wa sera ya jinsi ya kuoanisha biashara isiyo rasmi baina ya nchi na malengo ya maendeleo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya iitwayo “kuirasimisha biashara isiyo rasmi barani Afrika” 'mapato kupitia biashara hiyo isiyo rasmi , ambayo wala haizingatii kodi za ndani na sheria nyingine, ni kati ya asilimia 20 na asilimia 70 ya ajira katika bara la Afrika.

Ripoti inapendekeza kwamba kuiimarisha na kuifuatilia mara kwa mara kunaweza kuinua ustawi endelevu na kuboresha kwa kiasi kikubwa matarajio, hasa kwa wanawake ambao huwa sehemu kubwa ya wafanyabiashara wasio rasmi, wakiwa ni zaidi ya nusu ya Afrika Magharibi na ya Kati na karibu asilimia 70 Kusini mwa Afrika.

Afisa wa uchumi wa FAO na mwandishi wa ripoti hiyo, Suffyan Koroma, amesema "Kuwezesha urasimishaji ndio chaguo pekee la sera ya Afrika kwa ajenda ya mabadiliko ili kutimiza malengo yake.”

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter