Fistula si ulozi wala laana, nenda hospitali utibiwe- UNFPA

Fistula si ulozi wala laana, nenda hospitali utibiwe- UNFPA

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA limekaribisha hatua ya Wizara ya Afya ya kujipanga kutafiti hali ya Fistula nchini humo.

Akizungumza na Idhaa hii, meneja programu ya afya ya uzazi, mama na mtoto UNFPA Felister Bwana amesema hatua hiyo itatoa fursa ya kuandaa mpango mkakati unaolenga kutibu na kutokomeza fistula akisema..

(Sauti ya Felista)

Na kuhusu fikra potofu kuwa mwenye Fistula amelogwa,  Bi. Bwana amesema..

(Sauti ya Felista)

Bi. Bwana ametaja hospitali kadhaa zinazotibu Fistula nchini Tanzania kuwa ni pamoja na CCRBT jijini Dar es salaam, Bugando mkoani Mwanza na Seliani huko Arusha.