Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kukabili ukosefu wa usawa wa kijinsia katika kukabili majanga wazinduliwa

Mpango wa kukabili ukosefu wa usawa wa kijinsia katika kukabili majanga wazinduliwa

[caption id="attachment_311489" align="aligncenter" width="615"]hapanapalemajanga

Mkutano wa kupunguza majanga ukianza nchini Mexico hii leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake UN Women limezindua mpango wa kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika kupunguza majanga, kwa kuzingatia kwamba wanawake na watoto huathirika zaidi wakati majanga hayo yanapozuka.

Shirika hilo limesema wanawake wengi zaidi ya wanaume walipata Ebola au kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo ulipozuka Afrika ya Magharibi mwaka 2016 kutokana na jukumu lao kubwa kama watoa huduma kwenye jamii zao.

Wakati huo huo nchini Bangladesh wanawake na wasichana ndio wanaoathirika zaidi kunapoanza msimu wa monsoon kwa sababu wengi wao hawawezi kuogelea au kuondoka kwenye nyumba zao kutokana na vikwazo vya kitamaduni limeongeza shirika hilo.