Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fahamu umuhimu wa huduma ya Kangaroo kwa mtoto njiti: Sehemu ya pili

Fahamu umuhimu wa huduma ya Kangaroo kwa mtoto njiti: Sehemu ya pili

Huduma ya Kangaroo ambayo hujulikana pia kama huduma ya ngozi-kwa-ngozi ni huduma iliyoanzishwa miaka ya 70 kuokoa maisha ya watoto njiti katika sehemu ambazo vifaa vya unyevunyevu kwa mtoto njiti au incubator havipatikani au kutumika. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linasema watoto hawa njiti huzaliwa na miili dhaifu na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kupoteza maisha yao iwapo hawatapa huduma hii kwa haraka na kwa usanifu.

Katika sehemu ya pili ya mahojiano haya, Amina Hassan anamuuliza Dkt. Asia Hussein, Meneja wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa UNICEF nchini Tanzania, huduma hii inamaanisha nini?