UM wadhamiria kurejesha amani Mali:Guterres

24 Mei 2017

Mashambulizi dhidi ya walinda amani nchini Mali hayatodhoofisha azma ya Umoja wa Mataifa kusaidia nchi hiyo katika dhamira yake ya amani ya kudumu ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, António Guterres amelaani vikali shambulio la Jumatano mjini Kidali lililokatili maisha ya walinda amani wawili kutoka Chad waliokuwa wakihudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA. Pia amemtakia ahueweni ya haraka mlinda amani aliyejeruhiwa katika shambulio hilo.

Nao wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameongeza sauti yao kwa kulaani shambulio hilo la kigaidi ambapo kundi linalounga mkono Uislam na Waislam “Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin, limedai kuhusika.

Wajumbe hao wametoa wito kwa serikali ya Mali kuchunguza mashambulio na kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria wakisisitiza kwamba kuwalenga walinzi wa amani kunaweza kuwa ni uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter