Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 400,000 hatarini kukumbwa na unyafuzi DRC

Watoto 400,000 hatarini kukumbwa na unyafuzi DRC

Mzozo unaoendelea kwenye eneo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, unaweka watoto wapatao 400,000 hatarini kupata utapiamlo mkali au unyafuzi. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Flora)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa taarifa hizo hii leo likisema kuwa ukosefu wa usalama umesababisha vituo vya afya katika majimbo matano kwenye eneo hilo la Kasai vifungwe.

Afisa wa UNICEF Patrick Rose amesema kufungwa kwa vituo hivyo kumekwamisha utoaji wa huduma za afya, sambamba na kufanyika kwa shughuli za kilimo na sasa hali ya lishe na huduma za kujisafi ni tete.

UNICEF imesema itahitaji dola milioni 40 kwa ajili ya operesheni zake za dharura kwenye majimbo yote matano yaliyomo kwenye la Kasai.