Wanawake wawajibike kulinda amani

23 Mei 2017

Mmoja wa walinda amani mwanamke kutoka Tanzania Kapteni Mary Shayo ambaye ni kiongozi wa walinda amani wanawake nchini Sudan Kusini amesema wanawake wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa amani kwa ajili ya jamii zao.

Katika mahojiano maalum Kapteni Shayo aliyeko katika kikosi cha ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur, UNAMID na ambaye amekuwa katika kikosi hicho kwa mwaka mmoja anasema wakati wa machafuko wanawake na watoto huathirika zaidi.

Kapteni huyo ambaye ni mlezi wa walinda amani wanawake ametoa wito kwa wanawake akisema

( Sauti Kapteni Shayo)

Siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huadhimishwa tarehe 29 Mei kila mwaka.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter